Timu ya Wolves imepambana kiume na
kuiduwaza Liverpool kwa kuitundika magoli 2-1 na kutinga raundi ya
tano ya kombe la FA katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Anfield.
Richard Stearman aliwafanya wageni
Wolves waongoze ndani ya sekunde 53, baada ya kuachwa bila ya ulinzi
na kuunasa mpira wa adhabu wa Helder Costa.
Costa alimtengenezea nafasi Andreas
Weimann aliyemzunguka kipa wa Liverpool, Loris Karius na kuifanya
Wolves kuongoza kwa magoli mawili kabla ya mapumziko.
Mchezaji mwenye asili ya Kenya
Divock Origi aliifungia Liverpool goli pekee la dakika za mwisho.
Richard Stearman akifunga goli kwa mpira wa kichwa
Andreas Weimann akimzunguka kipa wa Liverpool na kufunga goli
Mshambuliaji Divock Origi akifunga goli pekee la Liverpool
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni