Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza timu
ya Chelsea imeitoa wapinzani wao wa London ya magharibi timu ya
Brentford na kutinga hatua ya tano ya michuano ya kome la FA kwa ushindi wa magoli 4-0.
Chelsea ilifanya mabadiliko ya
wachezaji tisa katika kikosi chake cha kwanza lakini walionekana kuwa
bora zaidi kuliko wapinzani wao.
Chelsea ilipata goli lake la kwanza
kupitia kwa Willian, kisha Pedro akafunga goli la pili katika kipindi
cha kwanza, Ivanovic akafunga goli la tatu na Michy Batshuayi
akafunga la nne kwa penati.
Pedro akifunga goli la pili la Chelsea katika mchezo huo
Michy Batshuayi akiruga juu kushangilia kufunga la nne kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni