Timu Denver Nuggets imemaliza gundu
la kufungwa michezo mitani na kuibuka na ushindi wa pointi 140-112
dhidi ya Indiana Pacers katika mchezo wa NBA Kimataifa uliochezwa
Jijini London, nchini Uingereza.
Nuggets ilianza kuimarika baada ya
Pacers kuongoza kwa pointi 31-30 mapema katika robo ya pili na
kumaliza mchezo huo kwa kupata pointi nyingi kuwahi kufungwa katika
msimu huu.
Katika mchezo huo Nikola Jokic
alifunga pointi 22 huku Denver ikimaliza rekodi ya Pacers ya kushinda
michezo mitano mfululizo katika dimba la London O2 Arena, mchezo
uliohudhuriwa na wachezaji nyota kadhaa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Wilson Chandler wa Nuggets akiwa kazini ambapo jana alifunga pointi 20
Jeff Teague akiruka juu kufunga pointi 2, ambapo jana alifunga jumla ya pointi 14
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni