Real Madrid imeweka rekodi mpya
nchini Hispania ya kucheza michezo 40, bila ya kufungwa baada ya
Karim Benzema kuokoa jahazi katika dakika ya 93 na kutoa sare ya 3-3
dhidi ya Sevilla katika michuano ya Copa del Rey hatua ya 16 bora.
Kikosi cha Zinedine Zidane,
kilichowapumzisha wachezaji wake nyota wengi katika mchezo huo,
ilifungwa mara ya mwisho na Wolfsburg katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali mchezo wa kwanza mwezi Aprili
2016.
Barcelona ilikuwa ikishikilia rekodi
ya kutofungwa michezo 39, waliyoiweka msimu wa mwaka 2015-2016 wakiwa
na Kocha Luis Enrique. Kwa sare hiyo ya jana Real Madrid imetinga
robo fainali kwa ushindi wa jumla wa magoli 6-3.
Beki wa Real Madrid Mbrazil Danilo akijifunga goli
Sergio Ramos akihamasisha mashabiki kushangilia kwa nguvu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni