Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria vikao vya bunge ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho jumanne.
Waziri mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayo pitia Dodoma kuelekea Kigoma.
Katika uwanja wa ndege, Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana pamoja na viongozi wa serekali na chama wa mkoa wa Dodoma.
Hivi karibuni Waziri Mkuu alizindua safari za ndege ya ATCL kati ya Dodoma na Kigoma
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni