Ndugu wawili wa familia ya Ayew wa
Ghana wamefunga goli kila mmoja katika ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
DRC Congo na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya
Afrika.
Mchezaji wa Aston Villa, Jordan Ayew
alikuwa wa kwanza kufunga goli katika dakika ya 62 kwa shuti la
kuzungusha katika dakika ya 62.
Paul-Jose M'Poku aliisawazishia DR
Congo kwa koli kali la shuti la mbali, lakini mchezaji wa West Ham,
Andre Ayew alifunga goli kwa mkwaju wa penati.
Jordan Ayew akiachia shuti la kuzungusha lililojaa wavuni na kuipatia Ghana goli la kwanza
Wachezaji wa Ghana wakishangilia goli kwa staili ya aina yake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni