Matumaini ya Arsenal katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya yanaelekea kuparanganyika baada ya kukubali kupata
kipigo ukome kunijua cha magoli 5-1 kutoka kwa Bayern Munich, katika
mchezo wa kwanza wa hatua ya 16.
Arsenal ambayo imekuwa ikitolewa
katika michuano hiyo katika hatua ya mtoano mara sita katika misimu
ya nyuma si tu ilikubali kipigo cha mkono, pali pia ilishuhudia
ikizidiwa na Bayern Munich ambayo ilimiliki mpira kwa asilimia 75.
Katika mchezo huo Alexis Sanchez
alirekebisha makosa yake ya kukosa kufunga kwa mkwaju wa penati, na
kufunga goli lililosawazisha goli lililofungwa na Arjen Robben kwa
shuti bora la umbali wa yadi 25.
Arsenal ilimkosa Laurent Koscielny
aliyeumia katika kipindi cha pili, huku Bayern ilicharuka ndani ya
dakika 10 ambapo Robert Lewandowski alifunga kwa kichwa huku Thiago
Alcantara akifunga mara mbili na kisha Thomas Muller kukamilisha
karamu ya magoli.
Arjen Robben akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Alexis Sanchez akifunga goli pekee la Arsenal katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni