Timu ya Real Madrid imetokea
kufungwa goli moja nyuma na kufanikiwa kuifunga Napoli magoli 3-1
katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16.
Wageni Napoli walipata goli la
kuongoza baada ya kipa Keylor Navas kushtukizwa na shuti murwa
lililopigwa na Lorenzo Insigne na kuandika goli ndani ya dakika nane.
Real Madrid ilisawazisha kupitia kwa
Karim Benzema kwa mpira wa kichwa, huku Toni Kross akiongeza la pili
kabla ya Casemiro kufunga goli la tatu.
Mpira uliopigwa kwa kichwa na Karim Benzema ukielekea golini
Nyota Cristiano Ronaldo akipoteza nafasi nzuri ya kufunga
Kama sarakasi vile: Karim Benzema akiruka juu ya kipa Pepe Reina
Kama sarakasi vile: Karim Benzema akiruka juu ya kipa Pepe Reina
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni