Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza na washiriki katika semina hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtela Mwampamba.
Baadhi ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilayani Kisarawe wakijadili changamoto za migogoro ya ardhi na nmna ya kuikabili. Semina hiyo iliandaliwa na TGNP Mtandao.
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda amewataka watendaji na viongozi wa vijiji vya wilaya hiyo kuakikisha wanatoa vipaumbele kwa wanawake katika umiliki wa ardhi na pia familia kuwashirikisha wanawake kutoa uamuzi pale wanapotaka kuuza ardhi mali ya familia. Bi. Seneda alitoa kauli hiyo alipokuwa akifunga semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya ya Kisarawe iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kujadilia matokeo ya utafiti raghibishi uliobaini uwepo wa migogoro mingi ya ardhi.
Kiongozi huyo amesema wanawake wengi wamekuwa wakiachwa nyuma katika suala zima la umiliki ardhi na wakati mwingine hata familia zimekuwa zikiuza ardhi kinyemela pasipo washirikisha wanawake jambo ambalo si la kiungwana.
"...Wakati mwingine unakuta mume anaamua kuuza ardhi hata bila kumshirikisha mkewe hili lazima viongozi mlisimamie, unapoletewa maamuzi ya familia kutaka kuuza ardhi waulizeni wanaume je wamewashirikisha wake zao katika uamuzi wa kuuza ardhi hiyo?," alisema Bi. Seneda akizungumza katika warsha hiyo.
Alitoa tahadhari kuwa endapo ataletea taarifa ya mwanamke katika wilaya yake kudhuumiwa ardhi na kiongozi au mtendaji wa kijiji kukaa kimya atahakikisha anaanza kumuwajibisha kiongozi kwa kufumbia macho dhuluma hiyo. Hata hivyo alisisitiza kuwa wanawake wana haki ya kumiliki ardhi kama ilivyo kwa wanaume hivyo viongozi wanapaswa kulisimamia suala hilo vizuri ili kundi hilo lisinyanyasike katika umiliki.
Aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi ngazi za juu kutatua migogoro ya ardhi ili kupunguza kero za wananchi na migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo hayo.
Aliwataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanashirikiana na wananchi na viongozi ngazi za juu kutatua migogoro ya ardhi ili kupunguza kero za wananchi na migogoro kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo hayo.
Alisema uongozi wake kwa kushirikiana na vyombo vingine wataendelea kufanya oparesheni za mara kwa mara kuhakikisha wanawaondoa wafugaji ambao wamekuwa wakivamia baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo na kulisha mifugo yao jambo ambalo limekuwa likileta migogoro na uharibifu wa mazao ya wakulima.
Bi. Bahati Magendo (wa kwanza kulia) mwakilishi wa wananchi Kijiji cha Vilabwa akizungumzia migogoro ya ardhi katika vijiji.
Kwa upande wake, Bi. Bahati Magendo mwakilishi wa wananchi Kijiji cha Vilabwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi na watendaji wa vijiji kuwapokea wafugaji kinyemela pasipo husisha wananchi jambo ambalo limekuwa likiendeleza migogoro baina yao na wafugaji.
Kwa upande wake, Bi. Bahati Magendo mwakilishi wa wananchi Kijiji cha Vilabwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi na watendaji wa vijiji kuwapokea wafugaji kinyemela pasipo husisha wananchi jambo ambalo limekuwa likiendeleza migogoro baina yao na wafugaji.
Alisema viongozi wamekuwa hawawashirikishi wananchi suala la kupokea wafugaji vijijini jambo ambalo limekuwa chanzo kikubwa cha migogoro. "..
Viongozi wanatudharau wananchi hasa sie akinamama wamekuwa hawatushirikishi katika maamuzi...utakuta mfugaji anakuja kijijini anazungumza na kiongozi kimya kimya baadaye anahamia sisi hatuambiwi chochote," alisema Magendo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni