Kostas Mitroglou ameipatia Benfica
goli moja katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya
16 katika mchezo dhidi ya Borussia Dortmund.
Mitroglou alifunga goli hilo muhimu
kwa mabingwa hao wa Ligi ya Ureno, kufuatia mpira wa kichwa uliopigwa
na Luisao katika kipindi cha pili.
Mchezaji wa Dortmund, Pierre-Emerick
Aubameyang, alipoteza nafasi ya kufunga pale mkwaju wake wa penati
alioupiga kumlenga kipa Ederson.
Kostas Mitroglou akishangilia kwa kukimbia baada ya kufunga goli pekee katika mchezo huo
Pierre-Emerick
Aubameyang akipiga penati iliyomlenga kipa na kudakwa
Sura ya kukosa penati: Pierre-Emerick
Aubameyang akisikitika kukosa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni