Angel di Maria amefunga mara mbili
wakati Paris St-Germain ikiipa kipigo cha paka mwizi timu ya
Barcelona na kuifanya kuwa katika hatari kutotinga hatua ya robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika muongo
mmoja.
Katika mchezo huo ambao PSG
iliutawala mno, ilipata goli lake la kwanza kwa mkwaju wa kuzungusha
wa adhabu uliopigwa kiufundi na Di Maria, na kisha Julian Draxler
aliongeza goli la pili.
Wakati Barcelona ikijiuliza Di Maria
tena akafunga goli la tatu kwa shuti la kuzungusha na mpira ukajaa
kwenye kona ya juu ya goli, kabla ya Edinson Cavani kukamilisha
ushindi huo kwa kufunga goli la nne na kufanya matokeo kuwa 4-0.
Angel di Maria akipiga kiufundi mpira wa adhabu uliozaa goli la kwanza
Julian Draxler akijipinda na kufunga goli la pili katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni