Timu ya Leicester City imepata
ushindi wake wa kwanza wakiwa nyumbani kwa mwaka 2017, baada ya goli
tamu la jitihada binafsi za Demarai Gray katika dakika za ziada
kuhanikiza ushindi dhidi ya Derby katika mchezo wa Kombe la FA,
mzunguko wa nne.
Alikuwa Andy King aliyewapatia
wenyeji goli la kwanza, kufuatia krosi iliyopigwa kiurevu na Gray,
lakini mpira wa adhabu uliopiga na Abdoul Camara ukafanya mchezo huo
uchezwa katika dakika za ziada.
Mchezaji aliyeingia akitokea benchi
Wilfred Ndidi katika mchezo huo ambao Leicester City ilishuka dimbani
ikiwa imefanya mabadiliko ya wachezaji 10, aliifungia goli la pili na
kisha Gray akamalizia la tatu.
Mchezaji Wilfred Ndidi akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni
Kipa wa Derby Jonathan Mitchel akiruka bila ya mafanikio kuufuata mpira uliopigwa na Wilfred Ndidi
Kinda Demarai Grayakishangilia baada ya kufunga goli la tatu la Leicester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni