Wachezaji Dimitri Payet na Memphis
Depay wamefunga magoli yao ya kwanza katika Ligi Kuu ya Ufaransa
almaarufu kama Ligue 1, tangu wahamie huko wakitokea Ligi Kuu ya
Uingereza mwezi Januari.
Aliyekuwa kiungo wa West Ham,
Dimitri Payet alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu, wakati timu
aliyojiunga nayo ya Marseille, ikiifunga Guingamp magoli 2-0.
Na aliyekuwa mchezaji wa Manchester
United, kiungo Memphis Depay aliyeingia akitokea penchi katika
kipindi cha pili aliifungia, wakati Lyon ikishinda kwa magoli 4-0.
Memphis Depay akiwapigia saluti mashabiki wa Lyon kwa kumkubali
Memphis Depay akipigwa buti ndani ya eneo la goli na kupatiwa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni