Timu ya Alaves imetinga fainali ya
Copa del Rey kwa mara ya kwanza katika historia yao ya miaka 96 baada
ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Celta Vigo katika mchezo wa
pili wa nusu fainali.
Winga Edgar Mendez alifunga goli
pekee katika michezo yao yote miwili waliocheza ya nusu fainali, pale
alipounyanyua mpira juu ya kipa Sergio Alvarez na kutikisa nyavu
katika dakika ya 83 ya mchezo.
Mchezaji wa zamani wa timu ya
Liverpool, Iago Aspas, alikaribia kuifungia Celta lakini mpira
alioupiga ulipanguliwa na kutolewa nje kipa Fernando Pacheco. Alaves
sasa watacheza fainali na mabingwa watetezi wa kombe hilo Barcelona.
Winga Edgar Mendez akifunga goli pekee katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni