Mwanamuziki Madonna ameposti kwenye
Instagram picha akiwa na watoto wakike mapacha aliowaasili kutoka
Malawi, akielezea kuwa amekamilisha mchakato na anafuraha kuwa nao
katika familia yake.
Katika ujumbe wake Madonna amesema
amefurahishwa mno na watu wote wa Malawi waliomsaidia kufanikisha
kuwapata mapacha hao wawili Stella na Esther. Mahakama nchini Malawi
jumanne ilitoa ridhaa kwa Madonna.
Madonna tayari anawatoto wawili raia
wa Malawi aliowaasili, ambao ni David, aliyemuasili mwaka 2006, na
Mercy, aliyemuasili mwaka 2009.
Binti wa Madonna Lourdes akiwa na mapacha wawili walioasiliwa na mama yake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni