Luis Suarez amefunga na kutolewa nje
kwa kadi nyekundu wakati Barcelona waliobakia tisa uwanjani wakitinga
fainali ya kombe la Copa del Rey, kwa ushindi wa matokeo ya jumla ya
magoli 3-2.
Suarez alifunga goli katika dakika
ya 43, kisha baadaye mchezaji wa Barcelona Sergi Roberto na Yannick
Carrasco wa Atletico Madrid wakatolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya
kupewa kadi mbili za njano.
Kevin Gameiro akitokea benchi
alikosa penati lakini baadaye akasawazisha makosa na kuisawazishia
Atletico Madrid. Suarez alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa
nje, na goli la Antoine Griezmann lilikataliwa kutokana na kuwa
ameotea.
Mabingwa watetezi Barcelona sasa
watakutana na ama Alaves au Celta Vigo katika fainali, baada ya timu
hizo kukutana hii leo katika mchezo wao wa pili wa nusu fainali ya
kombe la Copa del Rey.
Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga goli katika mchezo huo
Lionel Messi akiugulia maumivu baada ya kukatwa buti katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni