Timu ya Bayern Munich imetinga robo
fainali ya kombe la Ujerumani kwa kuifunga Wolfsburg kwa goli 1-0.
Goli la Bayern lilifunga Douglas
Costa kupitia shuti lililojaa wavuni baada ya kugongwa na Luiz
Gustavo.
Kipa wa Bayern Manuel Neuer aliokoa
goli lake mara mbili na kumyima fursa ya kutikisa nyavu Yunus Malli
katika dakika za mwisho.
Katika mchezo mwingine wa kombe hilo
Hamburg iliifunga Colgne magoli 2-0, Borussia Monchengladbach
wakaifunga Greuther Furth 2-0.
Douglas
Costa akijipinda na kufunga goli pekee katika mchezo huo
Robert Lewandowksi akidibitiwa na mabeki wa Wolfsburg
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni