Licha ya rais Donald Trump kutaka
sheria ngumu za uhamiaji na kukabiliana na ugaidi, lakini ikija suala
la taulo za bafuni za kwenye ndege yake ya Air Force One, anaonekana
kupendelea taulo laini zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizovuja
Ikulu ya Marekani, kiongozi huyo imara wa Marekani, ameonekana
kukerwa na ugumu wa taulo za mikono kwenye ndege yake, kiasi cha
kulalamikia wasaidizi wake.
Na hilo sio stori pekee kumhusu
Trump, kwa mujibu wa The Huffington Post, rais huyo pia hapendi
kusoma rundo la ripoti ambapo amewaagiza wasaidizi kufupisha ripoti
hizo na kuziweka katika ukurasa mmoja tu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni