Matumaini ya Tottenham katika ligi
ya Uropa yamepata pigo baada ya Jeremy Perbet kufunga goli pekee
lililoipa Gent ushindi wa kushangaza katika mchezo wa wa kwanza wa
hatua ya 32 bora.
Mshambuliaji huyo Mfaransa Perbet
aliumiliki vyema mpira na kuutumbukiza kwenye kona ya goli na
kumuacha kipa wa Tottenham Hugo Lloris akiuangalia.
Kikosi imara cha Tottenham kilicheza
vibaya katika mchezo huo, licha ya jitihada za Harry Kane kuishia
kugonga mwamba.
Jeremy Perbet akiwa ameupiga mpira uliozaa goli pekee katika mchezo huo
Moussa Sissoko akianguka chini baada ya kujaribu kuunasa mpira
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni