Ushindi wa Italia wa magoli 2-0 dhidi ya Albania ulisubiri kwa dakika nane baada ya mashabiki wa
Albainia kurusha fashifashi na mabomu ya moshi katika dimba.
Katika mchezo huo kipa wa Italia,
Gianluigi Buffon alicheza mchezo wake wa 1,000, huku wakipata goli la
kuongoza kupitia kwa mkwaju wa penati ya Daniele de Rossi.
Urushaji wa fashifashi ulifanyika
kwanza wakati De Rossi akipiga penati, lakini ilikuwa katika kipindi
cha pili ambapo wachezaji walilazimika kutoka uwanja katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kombe la dunia.
Daniele de Rossi akimpoteza mahesabu kipa wa Albania na kufunga goli
Immobile akiangalia mpira aliopiga ukijaa wavuni na kuandika goli la pili
Mashabiki wa Albania wakiwa wamewasha fashifashi na kurusha mabomu ya moshi uwanjani
Kipa wa Italia Gianluigi Buffon akinyanyua mikono juu kuwashukuru mashabiki kwa kutimiza mchezo wake wa 1,000
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni