Kiungo David Silva amefunga goli
zuri na kuongeza rekodi yake ya kuifungia timu ya taifa lake ya
Hispania wakati wakiibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Israel.
Mchezaji huyo wa Manchester City
amefikisha magoli 29 akiwa na Hispania katika michezo 110, baada ya
kufunga katika dakika ya 13 ya mchezo.
Magoli mengine ya Hispania katika
mchezo huo wa kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia yalifungwa na
mshambuliaji nyota wa Chelsea, Diego Costa, Vitolo pamoja na Isco.
Mpira uliopigwa kiufundi na David Silva ukimpita kipa na kuelekea wavuni
Diego Costa akiupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli la tatu la Hispania
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni