Rais Donald Trump ameripotiwa
kukasirishwa na kitendo cha mkwewe ambaye ni mshauri wake mwandamizi
pamoja na binti yake kuwa katika mapumziko wakati wa kura muhimu ya
ya muswada wake wa afya.
Binti yake huyo Ivanka Trump na
mumewe Jared Kushner wapo huko Aspen pamoja na watoto wao wakifurahia
mapumziko yao kwa kucheza mchezo wa kuteleza kwenye barafu, wakati wa
maamuzi muhimu ya muswada huo.
Muswada huo wa afya wa Marekani,
umeshindwa kupita katika baraza la Congress licha ya kuwa na
wawakilishi wengi wa Republican, ambapo Spika Paul Ryan alilazimika
kuuondoa jana.
Ivanka Trump akiwa na mumewe Jared Kushner mapumzikoni huko Aspen
Ivanka Trump na mumewe Jared Kushner wakiteleza kwenye barafu huko Aspen
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni