Kiungo wa Tottenham, Dele Alli,
amefungiwa kucheza michezo mitatu ya michuano ya Ulaya baada ya
kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi ya Uropa dhidi
ya Gent.
Alli alitolewa nje kwa kadi mwezi
Februari baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Gent, Brecht Dejaegere, katika mchezo
ulioisha kwa sare ya 2-2.
Iwapo Tottenham itamaliza kwa
kushika nafasi tatu za juu katika Ligi Kuu ya Ungereza, Alli atakosa
nusu ya kampeni za michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Dele Alli akimchezea rafu mbaya mchezaji Dejaegere
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni