Kapteni wa Argentina Lionel Messi
ameifungia nchi yake goli katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Chile huko
Buenos Aires na kuimarisha matumaini ya Argentina kufuzu michuano ya
Kombe la Dunia.
Mchezaji wa Chile Jose Pedro
Fuenzalida alimuangusha Angel Di Maria kwa kumsukuma kwa nyuma na
kusababisha kutolewa penati.
Mfungaji nyota wa Argentina Lionel
Messi aliipiga penati hiyo kwa utulivu iliyompita kipa Claudio Bravo
ikiwa ni siku 269 kupita tangu akose penati dhidi ya Chile katika
finali ya Copa Amerika.
Angel Di Maria akilalamika kwa refa baada ya kusukumwa chini na Jose Pedro
Lionel Messi akiwa amempoteza mahesabu kipa Claudio Bravo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni