Timu ya Brazil imetokea nyuma
kufungwa goli moja na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-1
dhidi ya Uruguay katika mchezo wa kutinga michuano ya Kombe la Dunia.
Katika mchezo huo Brazil walifungwa
goli katika dakika ya tisa tu kufuatia penati iliyopigwa na mchezaji wa PSG Edinson
Cavani.
Paulinho aliyefunga magoli matatu
'hat-trck' katika mchezo huo alisawazisha goli na kuongeza mengine
kabla ya Neymar kufunga goli la nne.
Edinson
Cavani akifunga goli kwa mkwaju wa penati
Neymar akidhibitiwa kati kati ya msitu wa mabeki wa Uruguay
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni