Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi
wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu katika kikao kazi
cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana
na uhalifu na wahalifu hapa nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari
ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi wa
Polisi ACP Advera Bulimba amesema kikao hicho kitawakutanisha maofisa
wakuu wa makao mkauu ya Polisi, makamanda wa Polisi wa mikoa na
Makamanda wa vikosi bara na Zanzibar ili kujadili mafanikio na
changamoto zilizojitokeza katika utendaji katika kipindi cha mwaka
uliopita na kuweka mikakati mipya ya kupambana na uhalifu kwa mwaka
2017.
Aidha, Bulimba amesema mbali na
utaratibu wa mawasiliano ya kila siku katika kuimarisha usalama wa
raia na mali zao, Jeshi la Polisi pia lina utaratibu wa kukutana kila
mwaka kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu kukabiliana na wahalifu kwa
lengo la kuhakikisha kuwa usalama wa raia na mali zao unaendelea
kuimarika hapa nchini.
Katika kikao hicho Inspekta Jenerali
wa Polisi IGP Ernest Mangu atatoa maelekezo ya kiutendaji ambayo
lengo lake ni kuhakikisha kuwa kila ofisa, mkaguzi na askari
anawajibika kwa nafasi yake katika kuhakikisha uhalifu unapungua hapa
nchini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni