Kocha Gareth Southgate amepata
kipigo cha kwanza wakati Uingereza ikizamishwa kwa goli 1-0 dhidi ya
Ujerumani kwa goli lililofungwa kiufundi na Lukas Podolski katika
kipindi cha pili.
Southgate alikuwa hajafungwa katika
michezo minne tangu aitwae Uingereza kutoka kwa kocha Sam Allardyce,
na kushuhudia machungu hayo kutoka kwa mabingwa wa kombe la dunia.
Katika mchezo huo Adam Lallana
alipiga mpira uliogonga mwamba wa goli na shuti la Dele Alli
lilizuiwa na kipa Marc-Andre ter Stegen, katika kipindi cha kwanza.
Lukas Podolski akiwa haamini goli alilofunga kwa kufunika kwa mikono uso wake
Jamie Vardy akiwa amevaana na kipa Marc-Andre ter Stegen
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni