Viongozi wa Mataifa yaliyoathirika
hivi karibuni na mashambulizi ya kigaidi wamepaza sauti zao za
kuonyesha mshikamano na Uingereza kufuatia shambulizi la kigaidi
karibu na majengo ya bunge lililouwa watu watano na kujeruhi 40.
Katika shambulizi hilo lililotokea
jana na kutekelezwa na mshambuliaji mmoja aliyepigwa risasi na kufa,
baada ya kutumia gari kuwagonga watembea kwa miguu na kuwauwa watu
watatu na kisha kumchoma kisu na kumuua askari nje ya bunge.
Afisa aliyeuwawa ametambulika kuwa
ni PC Keith Palmer, 48, ambaye ameoa na ana watoto. Waziri Mkuu
Theresa May amesema muuaji ni mgonjwa na mtu wa hovyo.
Mtu aliyetekeleza mauaji hayo akiwa kwenye machela akipatiwa huduma ya kwanza
Watoa huduma ya kwanza wakipambana kujaribu kuokoa uhai wa mtu aliyetekeleza shambulizi la kigaidi eneo la Westminster Uingereza
Mwanaume mmoja aliyegongwa kwa gari akipatiwa msaada
Majeruhi mwingine aliyegongwa na gari na muuaji akipatiwa matibabu
Mwanamke aliyejeruhiwa kwa kugongwa na gari akipatiwa msaada
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni