Paulo Dybala amefunga magoli mawili
wakati Juventus ikiichakaza Barcelona kwa magoli 3-0 katika mchezo wa
kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Jijini
Turin.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina,
alifunga alifunga magoli hayo yote mawili kwa mipira ya kuzungushwa
katika kipindi cha kwanza na kuwapa wakati mgumu wageni Barcelona.
Katika mchezo huo Juventus ilitawala
na kuifanya Barcelona kujilinda zaidi hata hivyo walijikuta
wakiongezwa goli la tatu kwa mpira wa kichwa lililofungwa na Giorgio
Chiellini.
Mshambuliaji Paulo Dybala akifunga goli la kwanza
Paulo Dybala akitupia goli la pili katika goli la Barcelona
Giorgio
Chiellini akichupa kichwa na kufunga goli la tatu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni