Mchezo wa robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya baina ya Borussia Dortmund na Monaco umelazimika
kuharishwa jana usiku baada ya kutokea milipuko mitatu karibu ya basi
la timu ya Dortmund.
Kufuatia tukio hilo beki wa
Dortmund, Marc Bartra, anahitaji upasuaji baada ya kuvunjika mfupo wa
kiwiko pamoja na kuchomwa na vigae vya dirisha la basi.
Tukio hilo limetokea wakati timu ya
Dortmund ikitoka hotelini kuelekea katika mchezo wao huo wa kwanza wa
robo fainali dhidi ya Monaco. Polisi wamesema upo uwezekano kuwa
tukio hilo ni la kigaidi.
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakipiga simu huku wengine wakiongea baada ya kutokea tukio hilo
Polisi wakiwa na baadhi ya wachezaji wa Borussia Dortmund
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni