Neymar ametolewa nje ya uwanja
wakati Barcelona wakipoteza mchezo wao dhidi ya Malaga kwa magoli 2-0
na kushindwa katika jitihada za kufikia pointi sawa na vinara wa Ligi
ya La Liga Real Madrid.
Mabingwa hao watetezi wa La Liga
walikuwa wamepata nafasi ya kuweza kufikia pointi za Real Madrid
ambayo katika mchezo wa awali ililazimishwa sare ya 1-1 na Atletico
Madrid.
Hata hivyo shambulizi la kipindi cha
kwanza lililofanywa na mchezaji wa zamani wa Barcelona Sandro Ramirez
na shambulizi la dakika za mwisho la Jony Rodriguez yalitosha
kumaliaza Barcelona.
Katika mchezo huo mshambuliaji nyota
Neymar alitolewa nje katika dakika ya 65, baada ya kupatiwa kadi ya
pili ya njano.
Luis Surez akidhibitiwa na mabeki wa Malaga asilete madhara yoyote
Jony Rodriguez akiifungia Malaga goli la pili na kuizamisha Barcelona
Neymar JR akionyeshwa kadi nyekundu na refa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni