Chelsea imeendelea kuongoza Ligi Kuu
ya Uingereza kwa tofauti ya pointi saba, kwa kupata ushindi murwa wa
magoli 3-1 dhidi ya Bournemouth.
Ikiwa na shinikizo la Tottenham
ambayo iliifunga mapema Watford, wageni Chelsea walionekana kuanza
vyema mchezo huo baada ya kupata magoli mawili kipindi cha kwanza.
Hata hivyo Bournemouth, ambao
waligonga mwamba wa goli, walichomoa goli moja kupitia shuti la mpira
wa mbali la Joshua King.
Bournemouth waliaendelea kufanya
mashambulizi, lakini walikuwa Chelsea waliobahatika kufunga goli la
tatu kupitia mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Marcos Alonso.
Diego Costa akishangilia baada ya mpira alioupiga kutumbukizwa kimiani na Adam Smith aliyejifunga
Eden Hazard akiwa ametumbukiza kimiani mpira na kuandika goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni