Mshindi wa medali mbili za dhahabu
za Olimpiki mwanadada Nicola Adams amecheza mchezo wake wa kwanza wa
ngumi za kulipwa na kuanza kwa ushindi.
Adams mwenye umri wa miaka 34
amepata ushindi wa pointi 40-36 dhidi ya Muargentina Virginia Carcamo
katika pambano lililofanyika Jijini Manchester City.
Akiongelea pambano hilo Adams
amesema hakutaka kumaliza pambano hilo mapema kwa kuwa alikuwa
akitaka kutoa burudani kwa mashabiki wa ngumi.
Katika michezo ya ngumi za ridhaa
Adams alishinda medali ya dhahabu Jijini London mwaka 2012 na Rio
nchini Brazil mwaka 2016.
Nicola Adams akimpa konde la kulia bondia Virginia Carcamo
Bondia Nicola Adams akiendelea kumuadhibu bondia Virginia Carcamo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni