Iago Aspas ameendelea kufanya vizuri
katika ufungaji wakati Celta Vigo ikiwazamisha wakina Mbwana Samatta
na timu yake ya KRC Genk kwa magoli 3-2 katika mchezo wa fainali ya
Ligi ya Uropa uliochezwa Hispania.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool
amefunga goli lake la 22 katika kampeni ya kukisaidia kikosi cha
Eduardo Berizzo kupata goli moja muhimu la ziada dhidi ya KRC Genk ya
Ubelgiji.
Celta Vigo iliutawala mchezo huo
katika muda mwingi lakini walikuwa wageni KRC Genk ambao walianza
kufunga goli kupitia kwa Jean-Paul Boetius katika dakika ya 10 tu ya
mchezo huo.
Iago Aspas akijipinda kuachia shuti lililojaa wavuni na kufunga goli
Kiungo Pablo Hernandez akiruka juu na kuupiga mpira kwa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni