Cristiano Ronaldo amekiri kuwa
hakuwahi kufikiria atakuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100
katika michuano ya Ulaya, wakati alipoanza soka lakini amesema
amefurahishwa mno na mafanikio ya hayo.
Ronaldo alifikisha magoli hayo baada
ya kuifungia Real Madrid magoli mawili Alhamis katika mchezo wa
kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ulioishia kwa
ushindi wa magoli 2-1.
Mshambuliaji huyo Mreno alikabidhiwa
fulana ya kumbukumbu ya kufikisha idadi hiyo ya magoli na rais wa
Real Florentino Perez hapo jana kwa kufanikiwa kufikia idadi hiyo ya
magoli na yeye kusema amefarijika mno.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni