Korea Kaskazini imeionya Marekani
kutofanya uchokozi katika ukanda wake, na kusema kuwa ipo tayari
kujibu mapigo kwa kutumia silaha za nyuklia.
Matamshi hayo yamekuja wakati Korea
Kaskazini ikiadhimisha miaka 105 ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa
hilo Kim Il-sung.
Gwaride kubwa limefanyika Pyongyang
huku kukiwa na uvumi kuwa kiongozi wao Kim Jong-un ataangiza
kufanyika majaribio mapya ya nyuklia.
Miongoni mwa silaha mpya
walizozionyesha ni pamoja na nyambizi yenye uwezo wa kurusha
makombora yanayoweza kufikia mabara mbalimbali.
Maonyesho hayo ya uwezo wa kijeshi
yamefanyika huku kukiongezeka kwa hofu ya kuibuka vita, wakati ndege
za kivita za Marekani zikielekea katika ukanda huo.
Wanajeshi wanawake wakipita kwa mwendo wa kasi wakati wa gwaride hilo
Wanajeshi wa kiume wakipita kwa ukakamavu mbele ya kiongozi wa Kim Jong-un
Makombora makubwa yaliyobebwa kwenye vifaru yakionyeshwa mbele ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Vikosi mbalimbali vya jeshi vilionyesha ukakamavu wao katika gwaride hilo
Aina nyingine ya kombora lililobebwa kwenye gari likionyesha katika gwaride hilo
Kikosi hiki cha jeshi la Korea Kaskazini kikiwa katika mwendo wa kasi wakati wa gwaride hilo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni