Cristiano Ronaldo amemaliza kwa
kishindo ukame wa kutofunga magoli kwa miezi sita katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya wakati Real Madrid ikitokea nyuma na kuifunga Bayern
Munich magoli 2-1.
Ronaldo, ambaye anashikilia rekodi
ya kufunga magoli mengi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifunga mara
mbili, katika kipindi cha pili na kumaliza ukame wa saa 11 bila
kufunga goli katika ligi hiyo.
Bayern Munich walikuwa wa kwanza
kufunga goli kupitia kwa Arturo Vidal, lakini baadaye alipoteza
nafasi nyingi za kuongeza goli la pili ikiwa ni pamoja na kupiga
penati iliyotoka nje ya goli.
Arturo Vidal akifunga goli pekee la Bayern Munich
Cristiano Ronaldo akinyanyua mkono juu kushangilia goli alilofunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni