Kinda Kylian Mbappe ametikisa nyavu
mara mbili wakati Monaco wakipata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya
Borussia Dortmund katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Katika mchezo huo uliopaswa kuchezwa
juzi lakini ukahairishwa baada ya tukio la milipuko, Mbappe
alitumbukiza kimiani krosi ya Thomas Lemar kabla ya Sven Bender
kujifunga na kuwa 2-0.
Ousmane Dembele alichomoa moja
kupitia pande la Pierre-Emerick Aubameyang, lakini Mbappe tena
akafunga goli la tatu kisha Shinji Kagawa akafunga goli la pili la
Dortmund.
Kylian Mbappe akifunga goli la kwanza katika mchezo huo
Shinji Kagawa akifunga goli la pili la Borussia Dortmund
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni