Timu ya Leicester City imeikazia
Atletico Madrid katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya
kufungwa goli 1-0 katika mchezo wao wa kwanza wa robo fainali.
Atletico Madrid ilipata goli lake
pekee katika kipindi cha kwanza pale refa aliposema Marc Albrighton
amemfanyia madhambi Antoine Griezmann katika eneo la penati.
Hata hivyo picha za video za marudio
zilionyesha madhambi hayo yalifanyika nje ya boksi, hata hivyo
Griezmann alipewa penati na kufunga.
Antoine Griezmann akifunga goli pekee kwa mkwaju wa penati
Riyad Mahrez akijiangusha chini kutaka penati katika kipindi cha pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni