Uongozi wa Chelsea katika Ligi Kuu
ya Uingereza umepungua na kuwa tofauti ya pointi saba, baada ya
kupata kipigo cha kushtusha nyumbani cha magoli 2-1 kutoka kwa
Crystal Palace huku Tottenham ikiifunga Burnley.
Kikosi cha Antonio Conte kilikuwa
kimeshinda michezo yao 10 iliyopita katika dimba la Stamford Bridge
na kilikuwa hakijapoteza nyumbani katika michuano yoyote ile tangu
Septemba 16, kabla ya kipigo hicho.
Katika mchezo huo Chelsea ilikuwa ya
kwanza kuona nyavu baada ya Cesc Fabregas kutumbukiza kimiani mpira
wa krosi ya Eden Hazard baada ya dakika tano tu ya mchezo lakini
wakajikuta wanapoteza mapema.
Wilfried Zaha aliyekuwa katika
kiwango chake alifanya jitihada binafsi na kusawazisha goli kwa shuti
la sekonde 91 na baadaye akamtengenezea nafasi ya kufunga Christian
Benteke na kuifanya Crystal Palace kupata goli la pili.
Eden Hazrad akifunga goli pekee la Chelsea katika mchezo wa jana
Wilfred Zaha akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni na kusawazisha goli
Christian Benteke akifunga goli la pili na la ushindi kwa Crystal Palace
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni