Tottenham imepunguza pengo na vinara
wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea na kuwa pointi saba baada ya baada
ya kuifunga timu ngumu ya Burnley kwa magoli 2-0 katika dimba la Turf
Moor.
Wageni Tottenham walihaha kusaka
goli na hatimaye jitihada zao zilizaa matunda baada ya kupata goli
kupitia kwa Eric Dier baada ya wenyeji kushindwa kuizuia krosi ya
Christian Eriksen.
Vincent Janssen, alijikuta akiingia
katika orodha ya majeruhi watatu wa Tottenham baada ya kuumia
akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu na nafasi yake
kuchukuliwa na Son Heung-min ambaye alifunga goli la pili.
Eric Dier akifunga goli la kwanza la Tottenham
Son Heung-min akifunga goli la pili la Tottenham
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni