Liverpool imeongeza nafasi ya
kujihakikisha kumaliza katika nafasi za juu nne za msimamo wa Ligi
Kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Everton kwa magoli 3-1.
Sadio Mane aliipatia Liverpool goli
la kuongoza baada ya kugongeana vyema na Roberto Firmino na kuachia
shuti lililokwenda kujaa kwenye kona ya goli.
Matthew Pennington aliifungia
Everton goli la kusawazisha likiwa ni goli lake la kwanza akiwa na
Everton akicheza kwa mara ya kwanza katika msimu huu.
Coutinho aliwatoka wachezaji wa
Everton na kufunga kwa shuti la kuzungusha na kisha baadaye
akamtengenezea Divock Origi aliyetokea benchi na kufunga goli la
tatu.
Sadio Mane akiachia shuti na kufunga goli la kwanza la Liverpool
Countinho akipiga shuti la mpira wa kuzungusha na kufunga goli la pili
Sadio Mane akichezewa rafu na Tom Davies ambaye alipewa kadi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni