Everton imepata ushindi wake wa saba
mfululizo wakiwa katika dimba la nyumbani huku Romelu Lukaku akitupia
wavuni mawili na kuizamisha Leicester City kwa magoli 4-2 ikiwa ni
kipigo cha kwanza kwa kocha Craig Shakespeare.
Alikuwa Tom Davies aliyewafungia
wenyeji goli la kwanza katika sekundi ya 30, kabla ya Leicester
kucharuka na kufunga kupitia Islam Slimani na kuongeza la pili
kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Marc Albrighton.
Lukaku alifunga kwa kichwa mpira wa
krosi ya Ross Barkley na kufanya matokeo kuwa 2-2 kabla ya Phil
Jagielka kuachiwa nafasi ya kutosha na kuiadhibu Leicester kwa
kufunga goli la tatu, na kisha baadaye Lukaku akaongeza la nne.
Romelu Lukaku akifunga goli kati ya magoli yake mawili
Mpira wa adhabu uliopigwa na Marc Albrighton ukitinga wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni