Matumaini ya timu iliyochini ya
msimamo wa ligi Sunderland kujinasua kushuka daraja yamepata pigo
jana baada ya Manchester United kuzidi kuisukumia chini kwa kuifunga
magoli 3-0.
Katika mchezo huo wa jana Sunderland
ilijikuta ikicheza na wachezaji 10 kwa zaidi ya dakika 45 baada ya
Sebastian Larsson kupewa kadi yenye utata kwa kumchezea rafu Ander
Herrera.
Zlatan Ibrahimovic alikuwa wa kwanza
kuipatia United goli la kuongoza kwa shuti la umbali wa yadi 20,
kabla ya kutolewa Larson, Henrikh Mkhitaryan alifunga la pili na
Marcus Rashford kumalizia la tatu.
Zlatan Ibrahimovic akiachia shuti na kufunga goli la kwanza la Man U
Marcus Rashford akijipinda kupiga mpira uliozaa goli la tatu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni