Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka
67 amenusurika kufa kwa kuning'inia kwenye gunia la unga wa mahindi
baada ya boti aliyokuwamo kuzama katika Ziwa Nyasa.
Graciam Kondowe alikuwa ni miongoni
mwa abiria 54 ambao polisi wamesema alinusurika baada ya boti
kupinduka kutokana na hali mbaya ya hewa.
Katika ajali hiyo iliyotokea jana
watu watano wamekufa maji na wengine 11 bado hawajulikano walipo kwa
mujibu wa polisi wa Malawi.
Boti hiyo ilikuwa imejaza waumini
waliokkuwa wametokea kwenye sherehe za Pasaka wakati ilipozama katika
eneo la lando la Wilaya ya Rumphi kaskazini mwa Malawi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni