.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Aprili 2017

KAHAWA YENYE UBORA WA KIMATAIFA KUZINDULIWA NCHINI

Dar Es Salaam, April 2017: DMG Tanzania, kampuni tanzu ya chakula na vinywaji nchini, imezindua bidhaa yenye mchanganyiko wa kahawa, maziwa na sukari ya  “Nuru coffee Chapchap” yenye hadhi ya kimataifa na ladha thabiti.

Uzinduzi huu umekuja wakati muafaka kufuatia changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea nchini ikiwa na dhumuni la kulenga kila Mtanzania kuonja ladha mpya ya Nuru coffee Chap chap ikipatikana nchini kote nchini na katika masoko yote.

Kutokana na ubunifu wa DMG Tanzania unaowatofautisha na wapinzani wake katika soko, kampuni hii imewawezesha  Watanzania hata ya hali ya chini, kuwa na uwezo wa kuonja ladha murua  yenye mchanganyiko wa maziwa, sukari na kahawa kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh 500=/

Akizungumzia  bidhaa hiyo mpya ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa Nuru Coffee Chapchap anasema “ Nuru coffee Chapchap ni bidhaa ya kipekee na ni moja kati ya bidhaa madhubuti katika kampuni yetu. Nuru ni neno la Kiswahili linamaanisha “mwangaza” ikiwa na maana ya asili, Nishati, na matumaini . Nuru huondoa giza na kuweka dhahiri vitu vilivyofichika. Nuru hung’aa popote na kurudisha tumaini kwa watu waliokata tamaa.”

Hivyo uzinduzi wa kahawa ya Nuru coffee Chapchap imekuja kwa wakati muafaka na kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa za ajira zinazotolewa nchini na kampuni hii na pia bidhaa ya nuru coffe imekuwa nuru kwa watanzania kwani imewawezesha  kujipatia chai yenye mchanganyiko wa sukari maziwa na kahawa kwa gharama nafuu kabisa kwa kuzingatia hali yetu uchumi.

Tunayofuraha kubwa kuzindua bidhaa hii ya kiwango cha juu itakayokidhi maisha ya mtumiaji, kwa kumpatia ladha nzuri ya kahawa bora kabisa na chapchap. Nuru coffee Chapchap inatokana na aina mbili kuu za kahawa nchini, Robusta na Arabika kwa asilimia 100 na kutengenezwa kwa mchanganyiko madhubuti wa maziwa na sukari, ili kuleta ladha nzuri ya kuvutia. Tumejipanga na tuna ujasiri mkubwa juu ya bidhaa yetu mpya na hivyo hatutatetereka.” Alisema ,Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni hiyo.

Hivi sasa Nuru coffee Chapchap inapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Dodoma na Arusha, na pia bidhaa hii inatarajiwa kupatikana mikoa mingine nchini miezi michache baadae.

Katika kusherekea uzinduzi wa Nuru Coffee Chapchap  katika soko la nchini 
Tanzania kampuni ya DMG Tanzania  imeandaa  kampeni itakayohusisha supamaketi kubwa mbalimbali kama TSN Supermarkert iliyopo kibo complex, 
American Super Markert pugu road na Nakumatt Mlimani City. Kampeni hiyo pia itahusisha  upatikanaji wa nuru Coffee katika mitaa mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 – 25 Aprili mwaka huu.

Kitu kikubwa Zaidi katika bidhaa ya Nuru coffe ni utaalamu wa usindikaji wa bidhaaa hiyo na ufungaji wa paketi zake  zinazolenga kuibua  hisia ya mtumiaji kabla hata hajainunua.

Nuru coffee Chapchap wafurahia kumtaja na kumtambulisha George Sixtus Mdemu, (G Nako) ambaye ni mwanamuziki wa kizazi kipya “maarufu kama Bongo Fleva” kuwa balozi wa bidhaa ya Nuru Coffee Chapchap nchini Tanzania. G Nako atakuwa akiitangaza bidhaa  ya Nuru coffee Chapchap katika soko la Tanzania pamoja na vyombo vya habari kama radio, TV, magazeti na mitandao ya kijamii.

Pamoja na mambo mengine G Nako kama balozi wa Nuru coffee Chapchap atakuwa akishirikiana pamoja na wateja wetu kueneza bidhaa yetu yenye ubora wa hali ya juu.

Tunayo furaha kubwa na tunategemea G Nako ataeneza uwezo wa bidhaa  yetu na kuwa balozi madhubuti. Tunajivunia kazi tunayoendelea kufanya pamoja naye na tunategemea kuimarisha uhusiano wetu kwa kuikuza lebo yetu na kuieneza kote nchini”  Alisema Bw. Rayton Kwembe Mkurugenzi wa kampuni hiyo.

Mimi pamoja na Nuru coffee Chapchap tumekuwa na uhusiano thabiti, DMG Tanzania ni kampuni nzuri na ninajivunia kufanya kazi pamoja nayo, “ G Nako.

DMG Tanzania haitabaki nyuma katika kuhakikisha inaongeza ubora katika bidhaa yake ya Nuru coffee Chapchap na pia inampango wa kuzindua bidhaa nyingine nyingi chini ya mwamvuli wa lebo ya Nuru. Ikiwa na lengo la kukuza usambazaji wa bidhaa yake DMG Tanzania inalenga kuifikia Tanzania yote pamoja na Africa Mashariki.
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni