Nyota wa zamani wa Uingereza na
Aston Villa, Ugo Ehiogu, amefariki dunia leo baada ya jana kupatwa na
shambulizi la moyo katika viwanja vya mazoezi vya Tottenham.
Kocha huyo wa Tottenham kwa
wachezaji chini ya miaka 23, alianguka jana asubuhi katika uwanja wa
maozoezi wa timu hiyo na kupatiwa huduma ya haraka na madaktari wa
Tottenham.
Madaktari wahuduma ya kwanza
waliitwa na alikimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa, lakini
alifariki dunia mapema leo akiwa na umri wa miaka 44.
Kocha Ugo Ehiogu akiwa na mkewe Gemma pamoja na mtoto wao wa kiume wakati wa uhai wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni