Polisi nchini Thailand imemkamata
mwanaume mmoja akijaribu kuingiza kwa njia za magendo vichupa sita
vyenye mbegu za kiume za binadamu nchini Laos.
Mamlaka za Thailand zilibaini chupa
kubwa ya gesi ya Nitrogeni kwenye begi la mtu huyo ikiwa na vichupa
hivyo wakati akikatiza katika mji wa Kaskazini mwa Thailand wa Nong
Khai.
Polisi wamesema mwanaume huyo
amethibitisha kuwa vichupa hivyo vilikuwa na mgegu za kiuume kwa
ajili ya Kiliniki ya tiba utungaji mimba Jijini Vientiane nchini
Laos.
Mtuhumiwa huyo Nithinon
Srithaniyanan, 25, alidakwa na polisi baada ya kumshuku kutokana na
kuvuka mpaka mara kwa mara akiwa na begi kubwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni