Goli la dakika za ziada lililofungwa
na Marcus Rashford limeipeleka Manchester United katika nusu fainali
ya Ligi ya Uropa na kuitoa Anderlecht katika mchezo uliofanyika Old
Trafford.
Ligi hiyo ya Uropa ni muhimu kwa
Manchester United na kocha Jose Mourinho anaitumia ligi hiyo kama
uwezekano wa kuelekea Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Manchester United walikuwa wa kwanza
kupata goli kupitia Henrikh Mkhitaryan katika dakika ya 10, lakini
goli hilo likasawazishwa baadaye na Sofiane Hanni.
Henrikh Mkhitaryan akiachia shuti lililozaa goli la kwanza
Sofiane Hanni akifunga goli pekee la Anderlecht katika mchezo huo
Zlatan Ibrahimovic akishikilia mguu wake baada ya kuumia goti
Marcos Rojo akiwa amebebwa kwenye machela baada ya kuumia na yeye
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni