Mcheza mieleka nyota John Cena
amepiga magoti jukwaani mbele ya watazamaji 70,000 akimuomba mpenzi
wake Nikki Bella amkubaliye kuwa mchumba wake.
Tukio hilo limefanyika baada ya Cena
na Bella kuwadunda maadui zao The Miz na Maryse, ambao ni wanandoa,
katika pambano la mieleka la wawili wawili.
Cena mwenye miaka 39 alianza kwa
kutoa mistari ya kumsifia Bella na kisha kupiga magoti ulingoni na
kutoa kiboksi chenye pete ya uchumba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni